KLABU ya Manchester City imetangaza rekodi mpya ya mapato yao kufikia paundi milioni 391.8, huku wakitengeneza faida kwa mwaka wa pili mfululizo. Vinara hao wa Ligi Kuu walitoa taarifa yao ya mwaka wa fedha wakionyesha kutengeneza faida ya paundi milioni 20.5 kwa msimu wa 2015-2016. Mwaka jana, City walitangaza mapato yao ya kwanza toka Sheikh Mansour alipochukua umiliki wa klabu hiyo mwaka 2008 na kuanza kuwekeza katika kikosi cha kwanza. Klabu hiyo ilitangaza hasara ya paundi milioni 197.5 msimu wa 2010-2011 ikiwa ni hasara kubwa kuwahi kupata klabu za Uingereza na kufuatia na hasara zingine za paundi milioni 97.9 msimu wa 2011-2012, paundi milioni 51.6 msimu wa 2012-2013 kabla ya hatimaye kutangaza ongezeko ya paundi milioni 11 msimu uliopita. Mapato ya paundi milioni 391.8 ya City ni ongezeko la asilimia 11 kulinganisha ya yale ya paundi milioni 351.8 waliyopata mwaka jana. Mapato hayo yamechangiwa kwa kiasi kubwa na upanuzi wa Uwanja wa Etihad ambao kwasasa unabeba mashabiki 55,000 na pia uwekezaji wa asilimia 13 wa kampuni mama ya China Media Capital Holdings.
No comments:
Post a Comment