MASHABIKI wa klabu ya FC Copenhagen waliwafurahisha watazamaji duniani kote kwa miwako na mafataki kuelekea mhezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Leicester City jana lakini walijisababishia matatizo kwa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA. Kueleka kuanza kwa mchezo huo uliofanyika Uwanja wa King Power, mashabiki wa Copenhagen waliosafiri kuishangilia timu yao waliwasha mafataki wakati wimbo wa mashindano hayo ukiimbwa muda ambao wachezaji wanaingia uwanjani. Hata hivyo, klabu hiyo sasa imeingia matatizoni kwa mashabiki hao kuvunja sheria kwa kuwasha mafataki hayo ambayo tayari yalishapigwa marufuku. Katika taarifa yake UEFA imedai kuwa kesi hiyo itashughulikiwa na kamati ya nidhamu ambayo itakutana Novemba 17 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment