MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger hadhani kama mustakabali wake unaweza kuathiri nyota wao Mesut Ozil na Alexis Sanchez kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. Ozil na Sanchez wote wamebakisha chini ya miaka miwili katika mikataba yao ya sasa lakini mazungumzo ya mikataba mipya tayari imeshaanza huku Arsenal wakitaka kuwapata ile ya muda mrefu. Wenger yuko katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na amesisitiza kuwa hatajadili mkataba mpya mpaka mwishoni mwa msimu na kufanya kuacha maswali mengi ya nani haswa atakuwa meneja wa klabu hiyo msimu ujao. Akihojiwa Wenger hadhani kama mjadala wa mkataba wake una mahusiano na ile ya kina Ozil na Sanchez kwani anaamini nyota hao wanafurahia kuwepo katika klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment