Monday, November 21, 2016

AC MILAN WAMUWINDA WILSHERE.

KLABU ya AC Milan inadaiwa kuwa na matumaini ya kumsajili kiungo wa Arsenal Jack Wilshere mwishoni mwa msimu huu. Kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza alipata nafasi ya kujiunga na timu hiyo kongwe nchini Italia majira ya kiangazi lakini aliamuakwenda kwa mkopo katika klabu ya Bournemouth. Toka atue Bournemouth Wilshere amefanikiwa kucheza mechi nane za ligi na anadaiwa kuwa tayari ameshakubali kuwa mustabali wake wa baadae unaweza kuwa nje ya Arsenal. Wilshere mwenye umri wa miaka 24 amekuwa akisumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara na kumfanya kufanikiwa kucheza mechi 105 pekee katika misimu tisa aliyocheza Arsenal. Milan wamepania kumsajili Wilshere kwa dili la moja kwa moja kipindi cha usajili wa kiangazi mwakani wakati ambao kiungo huyo atakuwa ameshamaliza mkataba wake.

No comments:

Post a Comment