Wednesday, November 30, 2016

ATLETICO NACIONAL YAIOMBA CONMEBOL KUWAPATA TAJI CHAPECOENSE.

KLABU ya Atletico Nacional jana wamelitaka Shirikisho la Soka la Amerika Kusini-CONMEBOL kuwapa taji la Copa Sudamericana wapinzani wao klabu ya Chapecoense ya Brazil kama heshima kwa wachezaji wa timu hiyo waliokufa katika ajali ya ndege. Klabu hiyo ya Colombia imetuma maombi hayo CONMEBOL kwa maandishi wakilitaka shirikisho hilo kuwapata taji hilo kwa heshima ya wale waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo. Chapecoense na Atletico Nacional zilikuwa zikutane leo katika fainali ya mkondo wa kwanza wa michuano ya Copa Sudamercana, michuano ya pili kwa ukubwa katika bara la Amerika Kusini baada ya ile ya Copa Libertadores. Taarifa kutoka CONMEBOL zilizotoka mapema ziliahirisha shughuli zote ikiwemo mchezo huo mpaka watakapotoa taarifa zaidi. Mamlaka nchini Colombia zinadai kuwa watu sita kati ya 81 ndio waliopona katika ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment