Thursday, November 24, 2016

BALE KUIKOSA EL CLASICO.

KLABU ya Real Madrid imethibitisha kuwa Gareth Bale anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wiki ijayo kufuatia majeruhi ya kifundo cha mguu yanayomsumbua na anatarajiwa kukaa nje kwa kipindi kirefu. Nyota huyo wa kimataifa wa Wales alipata matatizo hayo katika ushindi wa mabao 2-1 waliopata Madrid dhidi ya Sporting Lisbon katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliofanyika juzi. Mapema jana Madrid walibainisha kuwa bado wanafuatilia hali ya nyota huyo lakini leo zimekuja habari mbaya zaidi kufuatia taarifa kuwa atalazimika kufanyiwa upasuaji. Katika taarifa yao Madrid wamedai kuwa jopo la matabibu wa klabu hiyo wameamua kufamyia upasuaji nyota huyo ili kutibu tatizo lake hilo. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa Bale atafanyiwa upasuaji huo Jumanne ijayo.

No comments:

Post a Comment