Thursday, November 24, 2016

JELA YANUKIA KWA ETO'O KUFUATIA TUHUMA ZA KUKWEPA KODI.

VYOMBO vya habari vya Hispania vimedai kuwa, mshambuliaji nyota wa zamani wa Cameroon, Samuel Eto’o anaweza kukabiliwa na kifungo jela cha miaka zaidi ya 10. Taarifa hizo zinadai kuwa waendesha mashitaka nchini humo wanamtuhumu Eto’o kwa makosa ya ukwepaji kodi wakati akiwa Barcelona. Eto’o mwenye umri wa miaka 35 ambaye kwasasa anacheza katika klabu ya Antalyaspor ya Uturuki anatuhumiwa kuwa alikwepa zaidi ya euro milioni 3.46. Tuhuma zinakuja kufuatia Eto’o kudaiwa kukataa kuweka wazi mapato yake aliyokuwa akipata kupitia kwa wadhamini wake ikiwemo kampuni ya iliyokuwa ikimtengenezea viatu.

No comments:

Post a Comment