Thursday, November 24, 2016

GERRARD ATUNDIKA DALUGA ZAKE.

NAHODHA wa zamani wa kimataifa wa Uingereza na Liverpool, Steven Gerrard ametangaza kustaafu soka baada ya kucheza kwa miaka 19. Gerrard mwenye umri wa miaka 36, ameichezea Liverpool mara 710 akishinda mataji nane makubwa lakini alijiunga na klabu ya Los Angeles Galaxy ya Marekani mwaka 2015. Nguli pia anashika nafasi ya nne miongoni mwa wachezaji walioichezea Uingereza mechi nyingine zaidi akiwa amecheza mechi 114 huku akiwa nahodha mara tatu kati sita alizocheza katika michuano mikubwa. Akihojiwa Gerrard amesema anajiona mwenye bahati kupata uzoefu huo mkubwa katika kipindi chote alichokuwa akicheza soka. Nguli huyo aliendelea kudai kuwa akiwa chipukizi alitimiza ndoto zake za kuvaa jezi nyekundu maarufu za Liverpool wakati alipoitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza katika mchezo dhidi ya Blackburn Rovers Novemba 1998.

No comments:

Post a Comment