Thursday, November 24, 2016

TANANIA YASHUKA VIWANGO FIFA.

TANZANIA imeendelea kuporomoka zaidi katika viwango vya ubora vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Mwezi uliopita Tanzania iliporomoka kwa nafasi 12 mpaka kufikia nafasi ya 144 lakini safari hii hali imezidi kuwa mbaya kufuatia kushuka kwa nafasi 16 zaidi mpaka kufikia nafasi ya 160 duniani na nafasi ya 48 kwa upande wa Afrika. Kwa upande wa nchi za Afrika Mashariki Uganda bado wameendelea kuwa vinara kwa kushika nafasi ya 73 duniani na 18 kwa Afrika wakifuatiwa na Kenya waliopo nafasi ya 89 na 21 kwa Afrika. Rwanda wao wamepanda kwa nafasi sita mpaka nafasi ya 101 duniani na ya 27 kwa Afrika, wanafuatiwa na Burundi waliopo nafasi ya 133 duniani na 39 kwa Afrika. Kwa upande wa Afrika Orodha hizo zinaongezwa na Senegal walioko nafasi ya 33 baada ya kushuka nafasi moja wakifuatiwa na Ivory Coast walioshuka nafasi nne mpaka ya 34 na kulingana na Tunisia waliopanda kwa nafasi nne. Kwa upande mwingine Misri wamerejea tena katika tano bora baada ya kupata kwa nafasi 10 mpaka nafasi ya 36 wakifuatiwa na Algeria ambao wameshuka kwa nafasi tatu mpaka nafasi ya 38.

No comments:

Post a Comment