Wednesday, November 16, 2016

BARCELONA WAPATA MDHAMINI MPYA WA JEZI ZAO.

KLABU ya Barcelona inatarajiwa kuwa na jina jipya mbele ya fulana zao kuanzia msimu wa mwaka 2017-2018 baada ya kupata wadhamini wapya kampuni ya Rakuten ya Japan. Kampuni hiyo imesaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo wenye thamani ya euro milioni 220. Kampuni hiyo kubwa ya biashara kwa njia ya mtandao nchini Japan ilizinduliwa mwaka 1997 na kuanza kujitanua nje ya nchi hiyo kuanzia mwaka 2005 na sasa wanataka kuendelea kujitanua zaidi kwa kujitangaza kupitia klabu hiyo yenye jina kubwa duniani. Rakuten watachukua nafasi ya Qatar Airways waliokuwa wadhamini wakubwa wa Barcelona toka mwaka 2013. Qatar Airways wao waliongeza mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumalizika kwa msimu wa 2015-2016.

No comments:

Post a Comment