Wednesday, November 16, 2016

TIMUATIMUA YA MAKOCHA WA AFRIKA YAENDELEA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Congo, Pierre Lechantre ametimuliwa kibarua chake na kumfanya kuwa kocha wan chi kutimuliwa toka kuanza kwa michuano ya kufuzu Kombe la Dunia hatua ya makundi kwa upande wa Afrika mwezi uliopita. Congo walitandikwa na Uganda bao 1-0 Jumamosi iliyopita na kufuatia kupoteza pia mchezo wao wa kwanza dhidi ya Misri Octoba umewafanya kuburuza mkia wa kundi E wakiwa hawana alama yeyote. Nchi hiyo pia imeshindwa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon itakayofanyika Januari mwakani nchini Gabon. Uamuzi wa kutimuliwa umetangazwa baada ya Mfaransa kukutana na maofisa wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo jana. Lechantre amekuwa akiinoa Congo kwa karibu mwaka mmoja lakini amefanikiwa kupata ushindi mara moja katika mechi saba. Makocha wan chi nyingine waliotimuliwa baada ya timu zao kufanya vibaya katika mechi zao ufunguzi za makundi zilizofanyika Octoba ni pamoja na kocha wa Algeria, Gabon na Libya. Kocha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Ephraim Mashaba yeye amesimamishwa pamoja na ushindi wa timu yake dhidi ya Senegal kwa tuhumiwa kuwatukana maofisa wa shirikisho la soka la nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment