Wednesday, November 16, 2016

SOUTHGATE ADAI YUKO TAYARI KUINOA UINGEREZA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amesema ameonyesha anaweza kuhimili vishindo vya kuiongoza timu hiyo katika mechi mechi kubwa zenye shinikizo. Southgate mwenye umri wa miaka 46 anapewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya Sam Allardyce baada ya kumaliza mkataba wake wa kuisimamia nchi hiyo katika mechi nne bila kufungwa baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Hispania. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Southagate amesema anadhani katika mechi nne alizosimamia ameonyesha kuwa anaweza mikikimikiki ya kukiongoza kikosi cha nchi hiyo. Southagate alipewa mikoba ya muda akitokea katika kikosi cha nchi hiyo cha vijana chini ya umri wa miaka 21 baada ya kuondoka Allardyce aliyedumu kwa siku 67 pekee. Katika mechi zake alizosimamia kocha huyo alishinda mchezo wake wa kwanza ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Malta kabla ya kuja kupata sare ya bila kufungana na Slovenia na baadae kuwaadabisha mahasimu wao wa siku nyingi Scotland kw mabao 3-0 wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment