Wednesday, November 16, 2016

SPURS YAMNYATIA STURRIDGE.

KLABU ya Tottenham Hotspurs inadaiwa kufikiria kumuwania mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge katika usajili wa dirisha dogo Januari mwakani. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza ameshindwa kuonyesha makali yake Anfield msimu huu na hajafunga bao lolote katika Ligi Kuu mpaka sasa. Spurs nao wamekuwa na uhaba wa mabao huku Harry Kane akiwa amekosa kipindi kirefu kutokana na majeruhi wakati Vincent Janssen akiwa amefunga bao moja pekee toka atue akitokea AZ Alkmaar. Kufuatia kumkosa Sturridge majira ya kiangazi, meneja Mauricio Pochettino sasa yuko katika mikakati ya kutaka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji Januari ili awe kushindania taji la ligi.

No comments:

Post a Comment