Wednesday, November 16, 2016

IWOBI ADAI HAKUTEGEMEA KUITWA KIKOSI CHA KWANZA MSIMU HUU.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Nigeria, Alex Iwobi amesema alitegemea kupelekwa kwa mkopo na Arsenal kabla ya kuanza kwa msimu huu. Nyota huyo amedai kuwa kucheza katika kikosi cha kwanza katika kipindi hiki kwenye klabu hiyo kumekuja kama jambo la kushtukiza na kushangaza. Iwobi alijiunga na klabu hiyo akiwa mdogo na kukua taratibu kabla ya kuibuka katika kikosi cha wakubwa cha timu hiyo kwenye mchezo wa kirafiki majira ya kiangazi kilichopita. Meneja wa Arsenal aliamua kumuacha Iwobi na baada ya kucheza mechi 13 za Ligi Kuu msimu uliopita nyota huyo mwenye umri wa miaka 19 amejikuta akipata nafasi zaidi msimu huu. Akihojiwa Iwobi amesema kamwe hakutegemea kuwepo alipo hivi sasa kwani alishafikiria kuwa atapelekwa kwa mkopo ili kupata uzoefu zaidi kabla ya kuitwa kikosi cha kwanza. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa kutokana na Wenger kumuamini na kumpa nafasi atajituma kadri ya uwezo wake na kucheza kama ni mchezo wake wa mwisho.

No comments:

Post a Comment