Thursday, November 17, 2016

FA YADAI HAITAFANYA HARAKA KUCHAGUA KOCHA MPYA.

OFISA mkuu wa Chama cha Soka cha Uingereza-FA, Martin Glenn amesema hawatafanya uamuzi wa haraka katika kuchagua kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo pamoja na Gareth Southgate kupewa nafasi kubwa. Southgate mwenye umri wa miaka 46 aliteuliwa kuwa meneja wa muda Julai kwa ajili ya mechi nne za mwisho za Uingereza kwa mwaka huu na kufanikiwa kushinda mechi mbili na kutoa sare zingine mbili. Toka alipopewa mikoba hiyo baada ya kuondoka kwa Sam Allardyce kocha huyo ameonyesha ukaribu mkubwa na wachezaji huku mwenyewe akisema ameonyesha thamani baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Hispania Jumanne. Pamoja na hayo, FA wamedai watachukua muda kabla ya kutoa maamuzi ya kocha gani atapewa mikoba ya kuiongoza timu hiyo. Glenn amesema anafahamu kuwa Southgate anapewa nafasi kubwa lakini hawataweza kufanya maamuzi ya haraka kutokana na uzoefu walipata huko nyuma.

No comments:

Post a Comment