Thursday, November 17, 2016

BELLERINI KUIKOSA UNITED.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa Hector Bellerin anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki nne kufuatia majeruhi aliyopata katika mchezo wa dhidi ya Tottenham Hotspurs. Beki huyo wa kimataifa wa Hispania, alipata majeruhi hayo ya goti katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 kabla ya mapumziko kupisha mechi za kimataifa. Mapema leo Wenger aliwaambia wanahabari kuwa Bellerin anatarajiwa kuwa nje kwa muda wa wiki nne baada ya kuumia katika sekunde 10 za mwisho kwenye mchezo huo. Taarifa hizo sasa zitamfanya Wenger kufanya mabadiliko katika safu yake ya ulinzi katika safari yao ya Old Trafford kupambana na Manchester United Jumamosi hii. Mbali na kukosa mechi hiyo ya Old Trafford, Bellerini pia atakosa mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain na Basel, mechi za ligi dhidi ya Bournemouth, West Ham United, Stoke City na Everton na robo fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Southampton.

No comments:

Post a Comment