Thursday, November 17, 2016

BOLIVIA WAKATA RUFANI KUPINGA KUNYANG'ANYWA ALAMA.

CHAMA cha Soka cha Bolivia-FBF kimekata rufani kupinga uamuzi wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kuwakata alama katika mechi zao za kufuzu Kombe la Dunia kwa kosa la kumchezesha beki mzaliwa wa Paraguay Nelson Cabrera. Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Peru Septemba mosi na sare ya bila kufungana na Chile siku tano baadaye ziliondolewa katika rekodi na badala yae wapinzani wao hao wote walipewa ushindi wa mabao 3-0. FBF pia ililimwa faini ya dola 12,250 kwa kosa hilo. Cabrera alikuwa akicheza katika klabu ya Bolivar inayoshiriki Ligi Kuu ya Bilivia toka mwaka 2012 na pia aliitwa katika timu ya taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Marekani Mei mwaka 2016 kabla ya kuiwakilisha katika michuano ya Copa Amerika Juni. Hata hivyo, Cabrera anadaiwa aliwahi kuiwakilisha pia timu ya taifa ya Paraguay mwaka 2007 hivyo ushiriki wake katika mechi hizo za kufuzu Kombe la Dunia iligundulika kuwa sio halali ndio maana wakachukuliwa hatu hiyo. Baada ya kuthibitisha kukata rufani, FBF wamedai kuwa kamwe FIFA haijawahi kujifanyia uchunguzi yenyewe bila kupokea malalamiko kutoka upande wowote.

No comments:

Post a Comment