Tuesday, November 22, 2016

DESCHAMPS KUMUITA TENA BENZEMA UFARANSA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps amekiri kuwa Karim Benzema anaweza kumuita tena katika kikosi chake lakini amesisitiza kuwa mshambuliaji huyo wa Real Madrid atarejea pale tu atakapoona ana umuhimu. Benzema hakuitwa katika kikosi cha nchi hiyo katika michuano ya Euro 2016 ambapo Ufaransa ilitinga fainali katika ardhi yao ya nyumbani, kufuatia kashfa iliyokuwa ikimkabili dhidi ya mchezaji mwenzake Mathieu Valbuena. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 hajaiwakilisha nchi yake toka Octoba mwaka 2015 lakini Deschamps sasa yuko tayari kumjumuisha katika kikosi chake siku zijazo. Akihojiwa Deschamps amesema hana tatizo lolote na Benzema kwani ni mchezaji muhimu kwa Ufaransa lakini uamuzi aliochukua huko nyuma wa kumuacha ilikuwa ni kwa manufaa ya timu. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa anaweza kumuita tena Benzema siku za usoni lakini ni kama tu ataona kutakuwa na manufaa kwa timu.

No comments:

Post a Comment