Friday, November 18, 2016

FIFA KUZICHUKULIA HATUA UINGEREZA NA SCOTLAND.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limefungua mashitaka ya kinidhamu dhidi ya Uingereza na Scotland kwa kuvaa beji zenye kiua katika mechi yao ya kufuzu Kombe la Dunia ambayo iliangukia katika siku ya kuwakumbuka mashujaa wao. Wachezaji wa timu zote mbili walivaa beji nyeusi zenye kiua katika mchezo huo ambao Uingereza ilishinda mabao 3-0 katika Uwanja wa Wembley Ijumaa iliyopita. Sheria za shirikisho hilo zinakataza fulana za wachezaji kuwa na ujumbe wa kisiasa, kidini, picha au kauli zozote binafsi zisizohusiana na masuala ya soka. Wazo la wachezaji kuvaa beji yenye viua lilikuja kabla mataifa hayo mawili hayakutana Novemba 11, ambayo ndio siku ya kuwakumbuka mashujaa wao waliopoteza maisha katika vita mbalimbali.

No comments:

Post a Comment