Monday, November 21, 2016

GUARDIOLA AKIRI KUKOSEA KUMUACHA TOURE.

MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amedai kuwa pengine alifanya makosa kumuacha Yaya Toure na yuko tayari kumrejesha kiungo huyo katika kikosi cha timu hiyo kinachoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Toure aliitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Guardiola katika ushindi wa mabao 2-1 iliyopata City dhidi ya Crystal Palace huku akifunga mabao yote mawili. Awali ilionekana kama maisha ya Toure Itihad yamefikia ukingoni kutokana na sintofahamu iliyojitokeza baina ya Guardiola na wakala wake Dimitri Seluk lakini baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast kuomba radhi mambo yanaonekana kwenda sawa. Akiulizwa kama Toure anaweza kuongezwa katika kikosi chake Januari, Guardiola alikubali na kudai inawezekana na kama wakifanikiwa kufuzu hatua ya timu 16 bora atakutana na jopo lake la kuamua.

No comments:

Post a Comment