Wednesday, November 2, 2016

GUARIOLA, ENRIQUE, RANIERI KUGOMBEA TUZO YA KOCHA BORA WA MWAKA.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetoa orodha ya makocha 10 ambao watagombea tuzo ya Kocha bora wa Mwaka kwa mwaka 2016. Moja wapo ya majina yaliyotajwa katika orodha ni pamoja na Claudio Ranieri wa Leicester City, Pep Guardiola wa Manchester City na Luis Enrique wa Barcelona. Ranieri ametajwa katika orodha hiyo baada ya kuiongoza Leicester kutwaa taji lao la kwanza la khistoria la Ligi Kuu, wakati Guardiola yeye amejumuishwa kufuatia mafanikio aliyopata Bayern Munich kwa kutwaa taji la Bundesliga na DFB Pokal kabla ya kujiunga na City. Enrique ambaye alitwaa tuzo hiyo mwaka jana, yeye ameingoza Barcelona kutwaa mataji mawili ya nyumbani yaani La Liga na Kombe la Mfalme, kabla ya kwenda kushinda taji la Klabu Bingwa ya Dunia na Super Cup ya Hispania. Kwa upande mwingine Zinedine Zidane yeye ameingia kwenye orodha hiyo baada ya kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Super Cup ya UEFA akiwa na Real Madrid wakati Diego Simeone ambaye timu yake ya Atletico Madrid ilipoteza mchezo wa fainali ya Ulaya na yeye amejumuishwa kwenye hiyo. Makocha watatu ambao timu zao zilifanya vyema katika michuano ya Euro 2016 akiwemo Fernando Santos ambaye aliiwezesha Ureno kutwaa taji hilo, Didier Deschamps ambaye timu yake ya Ufaransa ilifika fainali na Chris Coleman aliyeifikisha Wales nusu fainali nao wametajwa kwenye orodha hiyo. Jurgen Klopp wa Liverpool na Mauricio Pochettino ndio majina yanayokamilisha orodha hiyo huku katika hali ya kushangaza Unai Emery ambaye aliiongoza Sevilla kuchukua taji lake la tatu mfululizo la Europa League kabla ya kwenda PSG, akiachwa katika orodha hiyo.

No comments:

Post a Comment