Wednesday, November 23, 2016

ISCO ATAKA MKATABA MWINGINE MADRID.


KIUNGO wa Real Madrid, Isco amedai kutaka kuongeza mkataba mpya na klabu hiyo yenye maskani yake Santiago Bernabeu. Nyota huyo amewahi kukaririwa kipindi cha nyuma akidai kuwa anaweza kuondoka Madrid ili aweze kupata nafasi zaidi ya kucheza seemu nyingine lakini katika wiki za karibuni ameimarika na kuwa mchezaji muhimu katika timu hiyo. Isco mwenye umri wa miaka 24 ameeleza kufurahishwa kwake na maendeleo yake na sasa anataka kuongeza mkataba mwingine na klabu hiyo. Akihojiwa Isco ambaye alikuwa akihusishwa na tetesi za kutakiwa Tottenham Hotspurs, amesema bado ana mkataba wa mwaka mmoja na nusu na Madrid lakini yeye pamoja na klabu wanataka kuongeza mkataba hivyo ana matumaini kila kitu kitakwenda sawa. Isco aliendelea kudai kuwa kwasasa anapata nafasi ya kucheza mara kwa mara hivyo anafurahia kwani anaisaidia timu.

No comments:

Post a Comment