Wednesday, November 23, 2016

KINDA LA GENK LATOA MASHARTI MAZITO KWA MAN UNITED.

WINGA wa klabu ya Genk, Leon Bailey amesisitiza kuwa atakataa nafasi ya kusaini Manchester United kama timu hiyo haitamuhakikishia nafasi ya kuwepo katika kikosi cha kwanza. Chipukizi huyo wa kimataifa wa Jamaica mwenye umri wa miaka 19, anatajwa kama mmoja wa wachezaji wanaovutia nchini Ubelgiji na amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwindwa na klabu kubwa. Paris Saint-Germain-PSG na Ajax Amsterdam zote zinatajwa kuwa zilijaribu kumsajili majira ya kiangazi wakati United nao pia wanaaminika kumfuatilia kwa karibu chipukizi huyo. Lakini Bailey mwenyewe ameweka wazi kuwa hana haraka yeyote ya kuondoka Genk kwasasa na kama akiondoka basi atakwenda katika klabu itakayoweza kumuhakikishia naafsi ya kucheza. Bailey amefunga mabao nane katika mechi 25 za mashindano yote alizocheza msimu huu.

No comments:

Post a Comment