Wednesday, November 30, 2016

KLOPP AAPA KUMLINDA WOODBURN.

MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema amedhamiria kumlinda Ben Woodburn baada ya chipukizi huyo kuvunja rekodi ya Michael Owen ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga bao katika klabu hiyo. Woodburn aliyeingia akitokea benchi akiwa na umri wa miaka 17 na siku 45, alifunga bao la pili la Liverpool katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Leeds United katika mchezo wa robo fainali ya Kombe Ligi. Akihojiwa Klopp amesema amefurahishwa na chipukizi huyo jinsi alivyoonyesha uwezo wake lakini tatizo moja kubwa analohofia ni vyombo vya habari ndio maana amekaa kimya. Woodburn aliibuka katika kikosi cha kwanza cha Liverpool katika ushindi waliopata dhidi ya Sunderland kwneye mchezo wa Ligi Kuu na siku tatu baadae amefanikiwa kuvunja rekodi ya Owen kwa kuipita kwa siku 98 huku mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Uingereza akiwa jukwaani akishuhudia. Klopp amesema chipukizi huyo bado ana mambo mengi ya kufanya na kuweka umaarufu wake pembeni kadrid awezavyo jambo ambalo anadhani litakuwa gumu.

No comments:

Post a Comment