MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger anahofu kiungo wake nyota Santi Cazorla anaweza kukaa nje ya uwanja kwa wiki 10 zaidi kutokana na majeruhi ya kifundo cha mguu yanayomsumbua. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania amekuwa nje ya uwanja toka Octoba baada ya kucheza mechi 11 katika mashindano yote msimu huu. Lakini Cazorla mwenye umri wa miaka 32 sasa anategemewa kuendelea kukaa nje zaidi kutokana na majeruhi kupona taratibu kuliko ilivyotegemewa awali. Wenger amesema Cazorla bado hajaanza hata kukimbia hivyo hadhani kama atarejea uwanjani hivi karibuni. Arsenal inakabiliwa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Swansea City baadae leo.
No comments:
Post a Comment