Saturday, January 14, 2017

CHELSEA, MAN UNITED ZAINGIA VITANI KWA BEKI WA LAZIO.

KLABU ya Chelsea inadaiwa kujipanga kupambana na Manchester United katika kipindi cha kiangazi kwa ajili ya kumuwania beki wa Lazio Stefan De Vrij. Beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi amekuwa akiwindwa kwa kipindi kirefu na United na sasa Chelsea nao wako tayari kuingia katika kinyang’anyiro hicho. Klabu ya Lazio imeondoa uwezekano wa kumuuza beki huyo katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo. Hatua hiyo imetoa mwanya kwa klabu hiyo kuweka kitita cha euro milioni 40 kwa timu itakayomuhitaji majira ya kiangazi.

No comments:

Post a Comment