Saturday, January 14, 2017

MAN UNITED KUMUONGEZA MKATABA DE GEA.

KLABU ya Manchester United inadaiwa kuwa tayari kuongeza mkataba wa mwaka mmoja uliopo katika mkataba wa David de Gea ili kuwakatisha tama Real Madrid. De Gea ambaye alisaini mkataba wa mpaka 2019 baada ya kushindwa kwenda Santiago Bernabeu Septemba mwkaa 2015, sasa ataongezwa mkataba wa mwaka mmoja zaidi pamoja na nyongeza ya mshahara. Kwasasa De Gea analipwa paundi 180,000 kwa wiki na kama akiongezwa mkataba huo utashuhudia akikunja kitita cha paundi 200,000 kwa wiki. Taarifa kutoka nchini Uingereza zimedai kuwa hakutakuwa na tatizo lolote katika nyongeza ya mkataba huo.

No comments:

Post a Comment