Wednesday, February 1, 2017

DORTMUND WAKANUSHA TETESI ZA REUS KWENDA ARSENAL.

MKURUGENZI wa michezo wa Borussia Dortmund, Michael Zorc amekanusha tetesi kuwa Marco Reus anajipanga kuondoka kwenda Arsenal mwishoni mwa msimu huu. Taarifa zilizozagaa kutoka nchini Ujerumani zimedai kuwa Arsenal inajipanga kumuwania Reus kama mbadala wa Alexis Sanchez ikiwa atakataa kusaini mkataba mpya, huku klabu hiyo ikidaiwa kuwa tayari kutoa mpaka euro milioni 60 kwa nyota huyo. Hata hivyo, Zorc alikanusha vikali tetesi hizo akidai kuwa hazina ukweli wowote kwani Reus mwenye umri wa miaka 27 hajawahi kuonyesha nia ya kuondoka. Akizungumza na wanahabari, Zorc amesema hawezi kuzungumzia suala hilo kwakuwa halina ukweli wowote. Reus alijiunga na Dortmund akitokea Borussia Monchengladbach mwaka 2012 na ana mkataba unaomalizika Juni mwaka 2019.

No comments:

Post a Comment