Thursday, February 2, 2017

MOURINHO ALIA NA WAAMUZI.

MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho amesema amekuwa akihukumiwa kwa sheria tofauti kulinganisha na mameneja wengine wa Ligi Kuu. Meneja huyo raia wa Ureno ameonekana kuchukukizwa na jinsi mwamuzi Mike Jones alivyochezesha mchezo wao wa jana ambao walitoka sare ya bila kufungana na Hull City. Akizungumza na wanahabari Mourinho amesema ni wazi wote wanafahamu yuko tofauti kwani hata sheria zinazochukuliwa dhidi yake ni tofauti. Katika mchezo wa juzi ambazo Liverpool walitoka sare ya bao 1-1 na Chelsea, meneja Jurgen Klopp alimfuata mwamuzi wa akiba Neil Swarbrick na kumuomba kwa kumkaripia na mwamuzi huyo alimsamehe. Kuafutia tukio hilo, Mourinho amesema kama angekuwa amefanya yeye hali ingekuwa tofauti na adhabu kubwa ingemshukia.

No comments:

Post a Comment