Thursday, February 2, 2017

KOCHA BURKINABE ALAUMU MWAMUZI KUFUATIA KUTOLEWA AFCON.

KOCHA wa timu ya taifa ya Burkina Faso, Paul Duarte amemlaumu mwamuzi Malang Diedhiou wa Senegal kufuatia kupoteza mchezo wao wa nusu fainali ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Misri jana huko Libreville, Gabon. Burkina Faso ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Misri baada ya dakika ya nyongeza na kwenda kupoteza kwa kufungwa mikwaju ya penati 4-3. Akizungumza na wanahabari, Duarte amesema mwamuzi ni sababu kubwa ya wao kupoteza mchezo wa jana kwani alikataa kuwapa penati ya wazi kufuatia mpira kushikwa eneo la hatari. Duarte aliwapongeza wachezaji wake kwa bidii kubwa waliyoonyesha huku pia akiwapongeza wapinzani wao Misri kwa kufanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment