Thursday, February 2, 2017

LAMPARD ATUNDIKA DALUGA.

KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Uingereza na Chelsea, Frank Lampard ametunga rasmi daluga zake na kuhitimisha miaka 21 ya kucheza soka. Nguli huyo mwenye umri wa miaka 38, ambaye mwaka jana alikuwa akicheza katika klabu ya New York City ya Marekani, ametangaza uamuzi wake huo kupitia ukurasa wa mitandao ya kijamii. Lampard ameitumikia Chelsea mechi 649 huku pia akiichezea Uingereza Uingereza mechi 106. Lampard amesema amepata ofa nyingi za kuendelea kucheza lakini akiwa amefikisha umri wa miaka 38 anadhani ni wakati muafaka wa kuanza ukuarasa mwingine katika maisha yake. Nguli huyo alikishukuru Chama cha Soka cha Uingereza-FA kwa kupitia vyeti vyake vya ukocha na sasa yuko tayari kutafuta shughuli nyingine nje ya uwanja.

No comments:

Post a Comment