Wednesday, February 1, 2017

LEICESTER YANASA BEKI WA MALI.

KLABU ya Leicester City, imemsajili beki wa kimataifa wa mali, Molla Wague kwa mkopo wa msimu mzima huku kukiwa na kipengele cha kusajiliwa moja kwa moja. Nyota huyo mwneye umri wa miaka 25 anajiunga na mabingwa hao wa Uingereza akitokea Udinese ya Italia. Wague anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na klabu hiyo kwa mwaka huu baada ya kiungo Wilfred Ndidi kusajiliwa mapema mwezi huu. Leicester walipokea kipigo chao cha 12 kutoka kwa Burnley jana na sasa wanashika nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi.

No comments:

Post a Comment