Wednesday, February 1, 2017

KOCHA WA BURKINA FASO ADAI MOURINHO NI KAMA BABA YAKE.

KOCHA wa timu ya taifa ya Burkina Faso, Paulo Duarte amebainisha kupigiwa simu na Jose Mourinho kuelekea mchezo wao wa nusu fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Misri baadae leo. Duarte amewahi kufanya kazi chini ya Mourinho wakati akianza soka na timu ya Uniao Leira mwaka 2001, na amekuwa akipewa hamasa kubwa na Mreno mwenzake huyo. Akizungumza na BBC Duarte amesema Mourinho alimpigia simu kumpongeza huku akidai kuwa hajashangazwa na kikosi chao kutinga hatua ya nusu fainali. Duarte aliendelea kudai kuwa Mourinho ni kama baba yake kwake na makocha chipukizi kutoka Ureno.

No comments:

Post a Comment