Wednesday, February 1, 2017

WENGER AJITETEA KUMUACHA BENCHI WALCOTT.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amejitetea kwa kutomuanzisha Theo Walcott katika mchezo wa Ligi Kuu waliofungwa mabao 2-1 na Watford jana, pamoja na kiwango bora alichoonyesha mwishoni mwa wiki iliyopita. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza aliibuka mchezaji bora wa mechi wakati walipoirarua Southampton kwa mabao 5-0, Mbapo Walcott alifunga hat-trick na Danny Welbeck akifunga mawili. Hata hivyo, Walcott alianzia benchi katika mchezo wa jana ambao Arsenal walijikuta wakiwa nyuma kwa mabao 2-0 katika kipindi cha kwanza. Akizungumza na wanahabari Wenger amesema uamuzi wa kumtumia Walcott kipindi cha pili ulikuwa wa kiufundi kwani bado wana mechi nyingi kubwa ambazo zinafuatana hivyo lazima achukue tahadhari. Arsenal kwasasa wako nyuma ya vinara Chelsea kwa alama tisa na wanatarajia kukutana nao Jumamosi hii katika Uwanja wa Stamford Bridge.

No comments:

Post a Comment