Wednesday, February 1, 2017

SWANSEA YAMNASA JORDAN AYEW.

KLABU ya Swansea City imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana na Aston Villa Jordan Ayew kwa mkataba ambao utashuhudia nyota wa kimataifa wa Wales Neil Taylor akihamia upande mwingine. Jordan amekuwa muhimili muhimu katika kikosi cha Ghana katika michuano ya Mataifa ya Afrika inayoendelea nchini gabon akiwa amefunga bao moja na kusaidia lingine moja. Swansea imetoa kitita cha paundi milioni tano pamoja na Taylor ili kuweza kupata saini ya nyota huyo ambaye wamempa mkataba wa miaka mitatu. Kwasasa Jordan akiwa na kikosi cha Ghana wanajiandaa kwa ajili ya mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Cameroon utakaochezwa kesho.

No comments:

Post a Comment