Friday, February 3, 2017

INIESTA, BUSQUET WAANZA MAZOEZI.

MENEJA wa Barcelona, Luis Enrique amepata ahueni kufuatia kurejea mazoezini kwa nyota wake Sergio Busquet na Andres Iniesta. Nyota hao wawili walikuwa wakisumbuliwa majeruhi, Busquet majeruhi ya kifundo cha mguu na Iniesta misuli ya kigimbi, lakini mapema leo wameanza mazoezi na wenzao. Uwezekano wao kuwepo katika mchezo wa kesho wa la Liga dhidi ya Athletic Bilbao bado haujaamuliwa lakini Enrique amewapa morali kwa kuwajumuisha katika maandalizi. Busquet amekosa mechi tatu za Barcelona wakati Iniesta yeye amekosa mechi nne mfululizo. Akizungumza na wanahabari Enrique amesema amefurahi kuwaona nyota hao wakirejea mazoezini lakini kuhusu suala la kucheza itategemea na taarifa ya mwisho watakayopata kutoka kwa madaktari. Barcelona walishinda bao 1-0 katika mchezo wao baina ya Bilbao uliochezwa Agosti mwaka jana.

No comments:

Post a Comment