Thursday, February 9, 2017

QATAR YATUMIA DOLA MILIONI 500 KILA KUJIANDAA NA KOMBE LA DUNIA 2022.

QATAR inatumia kiasi cha dola milioni 500 kila wiki kwa ajili ya miundombinu ya nchi hiyo ili kuhakikisha wanajiandaa vyema kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022. Waziri wa fedha wa Qatar, Ali Shareef Al-Emadi amesema kuwa zaidi ya dola bilioni 200 zitatumika kwa jumla katika ujenzi wa viwanja, barabara, uwanja mpya wa ndege na hospitali. Akizungumza na wanahabari Al-Emadi amesema wanatumia karibu dola milioni 500 kila wiki jambo ambalo linatarajiwa kuendelea kwa kipindi cha miaka mitatu minne ijayo ili kufikia malengo yao. Al-Emadi aliendelea kudai kuwa asilimia tisini ya ujenzi kwa ajili ya michuano hiyo tayari imefikia pazuri na hiyo sio kwa viwanja pekee bali hata barabara, reli, bandari, viwanja vya ndege na hata hospitali. Waziri huyo aliendelea kudai kuwa lengo lao kubwa ni kuhakikissha wanakuwa tayari kwa michuano hiyo kwa wakati na sio kuona watu wakipaka rangi wakati wageni wameshaanza kuingia.

No comments:

Post a Comment