Thursday, February 9, 2017

UEFA YATAKA TIMU 16 KOMBE LA DUNIA.

SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA linatarajia kuomba kupeta nafasi 16 kwa timu zake wakati michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2026 itakapoongezwa timu 48. UEFA pia wanatarajiwa kuomba timu za Ulaya ambazo zitafuzu kutenganishwa katika hatua ya kwanza ya makundi. Mfumo mpya wa michuano hiyo unatarajiwa kuwa na hatua ya makundi 16 yenye timu tatu huku timu 32 zikifuzu katika hatua ya mtoano. Timu 13 za Ulaya zilifuzu michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Brazil mwaka 2014 ambapo Ujerumani walishinda taji hilo.

No comments:

Post a Comment