Thursday, February 9, 2017

WENGER ATAKA MASHABIKI KUUNGANA.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza sio mustakabali wake uliopo katika mashaka bali msimu wa timu hiyo kufuatia kushuka kwa kiwango chao katika siku za karibuni. Wenger amekuwa akishambuliwa vikali kufuatia kichapo cha mabao 3-1 walichopata kutoka kwa vinara wa Ligi Kuu Chelsea, ikiwa ni mara ya pili baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Watford kwa mabao 2-1. Matokeo hayo yameifanya Arsenal kuwa nyuma ya Chelsea kwa alama 12 na kuzusha hasira kwa mashabiki ambao wanadhani muda wa kocha huyo kuondoka umefika. Akizungumza na wanahabari Wenger amesema mustakabali wake sio muhimu kwasasa, jambo la muhimu na kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya mchezo wao ujao dhidi ya Hull City.

No comments:

Post a Comment