Thursday, March 16, 2017

AHMAD AHMAD RAIS MPYA CAF, ZANZIBAR WAUKWAA UANACHAMA.

RAIS wa Shirikisho la Soka la Madagascar, Ahmad Ahmad amefanikiwa kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF akimshinda mpinzani wake Issa Hayatou wa Cameroon. Ahmad alishinda uchaguzi huo kwa kuzoa jumla ya kura 34 kati ya kura 54 za wajumbe huku mpinzani wake Hayatou ambaye ameiongoza CAF toka mwaka 1988 akiambulia kura 20. Uchaguzi huo umefanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia ambapo pamoja na mambo mengine Chama cha Soka cha Zanzibar-ZFA hatimaye nacho kimefanikiwa kupata uanachama rasmi CAF. ZFA ilikuwa imetuma maombi ya kutambuliwa kama mwanachama rasmi wa CAF na baada ya jopo la wajumbe wa mkutano huo kukutana walipitisha kwa kauli moja kulikubali ombi hilo la Zanzibar. Sasa CAF ambayo ilikuwa na wanachama 54 hapo awali kabla ya mkutano, itakuwa na jumla ya wanachama 55 huku Zanzibar wakiwa wanachama wapya.

No comments:

Post a Comment