Friday, March 17, 2017

FIFA YAIPIGA KUFULI MALI.

CHAMA cha Soka cha Mali-Femafoot kimesimamishwa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA mpaka itakapoamuliwa vinginevyo kufuatia serikali ya nchi hiyo kuingilia masuala ya soka. FIFA imechukua hatua hiyo baada ya Waziri wa Michezo wa Mali Housseini Amion Guindo kuvunja kamati ya utendaji ya Femafoot. Guindo pia aliteua kamati ya muda iliyopewa mamlaka ya kuongoza Femafoot mpaka uchaguzi mwingine utakapofanyika ndani ya miezi 12. Katika taarifa yake FIFA imedai kuwa marufuku hiyo itaondoshwa wakati bodi ya Femafoot iliyokuwepo awali itakaporejeshwa madarakani. FIFA iliendelea kudai hakuna timu yeyote kutoka Mali zikiwemo klabu zitakazoruhusiwa kushiriki michuano ya kimataifa kuanzia leo.

No comments:

Post a Comment