Wednesday, March 15, 2017

CAF YAMFUNGULIA MASHITAKA YA KINIDHAMU CHIYANGWA.

SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF linatarajia kumfungulia mashitaka ya kinidhamu dhidi ya rais wa Baraza la Soka la Nchi za Kusini mwa Afrika-Cosafa, Phillip Chiyangwa. Chiyangwa amekuwa akimponda Issa Hayatou na kujinasibu kuwa yeye ndiye kampeni meneja wa rais wa shirikisho la Soka la Madagascar, Ahmad Ahmad ambaye anashindana na Hayatou katika uchaguzi mkuu wa kesho. CAF imedai kuwa hatua za hivi karibuni zilizofanywa na Chiyangwa na kauli zinaonyesha kulikosea heshima shirikisho hilo, rais wake na wajumbe wa kamati ya utendaji. CAF imeamua kufungua kesi dhidi ya Chiyangwa mabaye ni rais wa Shirikisho la Soka la Zimbabwe katika kikao chao cha kamati ya utendaji kilichokutana jijini Addis Ababa, Ethiopia jana ikiwa zimebaki siku mbili kabla ya uchaguzi.

No comments:

Post a Comment