Monday, March 27, 2017

ARDA TURAN AUMIA AKIWA KWENYE MAJUKUMU YA KIMATAIFA.

SHIRIKISHO la Soka la Uturuki-TFF limethibitisha kuwa nahodha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Arda Turan amepata majeruhi ya nyonga na anatarajiwa kukosa mchezo w kirafiki wa kimataifa dhidi ya Moldova baadae leo. TFF walithibitsiha taarifa kufuatia nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 kuachwa katika kikosi cha nchi hiyo baada ya kushindwa kupona kwa wakati. Awali ilikuwa imeripotiwa kuwa majeruhi aliyopata Turan hayakuwa makubwa sana na kulikuwa na uwezekano wa kucheza mchezo wa Jumapili hii wa klabu yake ya Barcelona dhidi ya Granada. Hata hivyo, baada ya kufanyiwa vipimo imegundulika kuwa hataweza kucheza mechi hiyo ya leo ingawa anaweza kupona kwa wakati kwa ajili ya mchezo huo wa La Liga Jumapili.

No comments:

Post a Comment