Tuesday, March 28, 2017

MECHI YA IVORY COAST NA SENEGAL YAVUNJIKA KUFUATIA VURUGU.

MCHEZO wa kirafiki wa kimataifa wa kati ya Ivory Coast na Senegal ulilazimika kusitishwa kufuatia mashabiki kuvamia uwanjani jijini Paris. Timu hizo zilikuwa zimetoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 kwenye dakika ya 88 wakati kundi la mashabiki liliporuka uzio na kuingia sehemu ya kuchezea huku shabiki mmoja akionekana kumrukia nyota wa Senegal Lamine Gassama. Wachezaji walilazimikia kukimbia nje ya uwanja na mwamuzi Tony Chapron aliamua kusitisha mchezo huo huku zikiwa zimebaki dakika mbili mpira kumalizika. Bao la Senegal lilifungwa na nyota wa Liverpool Sadio Mane kwa penati huku lile la Ivory Coast likifungwa na Bi Gohi Cyriac. Mmoja wa mashuhuda wa mchezo huo amesema watu hao waliovamia uwanja hawakuwa na nia mbaya bali walitaka kuwa karibu na wachezaji ikiwemo kupiga nao picha lakini ni suala linalotakiwa kutizamwa kwa umakini kwani lolote linaweza kutokea.

No comments:

Post a Comment