Wednesday, March 29, 2017

BRAZIL YAWA NCHI YA KWANZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA.

BRAZIL imekuwa nchi ya kwanza kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 jana kufuatia ushindi wa mabao 3-0 waliopata dhidi ya Paraguay. Kikosi cha Brazil kinachonolewa na kocha Tite sasa kinaungana na wenyeji Urusi kuwa timu pekee ambazo mpaka ndizo zenye nafasi ya kushiriki michuano hiyo. Ushindi wa Brazil ulikuwa hautoshelezi kuwapa nafasi hiyo lakini kufungwa kwa Uruguay mabao 2-1 na Peru ndio iliyowapa rasmi nafasi hiyo. Brazil ilipoteza mechi yake ya kwanza ya kufuzu nchi za Amerika Kusini kwa Chile, lakini toka wakati huo wamecheza mechi 13 bila kupoteza na kuwafanya kukaa kileleni wakiwa na alama 33 baada ya kucheza mechi 14, wakishinda 10, sare tatu na kupoteza moja.

No comments:

Post a Comment