Wednesday, March 29, 2017

TEKNOLOGIA YA VIDEO KUMSAIDIA MWAMUZI YAANZA KUONYESHA MATUMAINI.

MFUMO wa teknologia ya video umetumika jana kusahihisha baadhi ya maamuzi katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki ambao Hispania ilifanikiwa kuifunga Ufaransa jijini Paris. Mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann bao lake lilikataliwa kufuatia picha za video za kumsaidia mwamuzi kuamua kwamba alikuwa ameotea. Mfumo huo pia ulikubali bao la pili la Hispania lililofungwa na Gerard Deulofeu baada ya mwamuzi wa pembeni kunyoosha kibendera kuwa alikuwa ameotea. David Silva ndiye aliyefunga bao la kuongoza kwa Hispania kwa penati baada ya Laurent Koscielny kumfanyai madhambi Deulofeu. Teknologia ya kutumia picha za video kumsaidia mwamuzi kwasasa iko katika majaribio, huku rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Gianni Infantino akitaka teknologia hiyo kutumika katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi mwakani.

No comments:

Post a Comment