Tuesday, March 28, 2017

MESSI AFUNGIWA MECHI NNE.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina, Lionel Messi anatarajiwa kukosa mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Bolivia baadae leo baada ya kulimwa adhabu ya kufungiwa mechi nne kwa kumtolea maneno machafu mwamuzi. Uamuzi huo umepelekwa Chama cha Soka cha Argentina saa chache kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya Bolivia huko jijini La Paz. Hatua hiyo imekuja kufuatia Messi kudaiwa kutumia lugha chafu dhidi ya mwamuzi msaidizi kwenye mchezo wao walioshinda bao 1-0 dhidi ya Chile Ijumaa iliyopita. Nyota huyo wa Barcelona pia ametozwa faini ya paundi 8,100 na anatarajiwa kukosa mechi za kufuzu dhidi ya Uruguay, Venezuela na Peru kabla ya kurejea kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Ecuador. Katika taarifa yake Shirikisho la Soka Duniani-FIFA limedai kuwa kamati yake ya nidhamu ndio ilifikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na tuhuma zilizotolewa.

No comments:

Post a Comment