Friday, March 10, 2017

CAF CHAMPIONS LEAGUE: YANGA KUIVAA ZANACO.

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga baadae leo wanatarajiwa kujitupa uwanjani kukwaana na Zanaco FC ya Zambia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga wamepata nafasi hiyo baada ya kuiondosha Ngaya de Mbe ya Comoro katika mzunguko wa awali na sasa wanacheza na Zanaco kutafuta nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa kabisa Afrika. Mchezo huo wa leo ambao utakuwa wa mkondo wa kwanza kabla ya ule wa marudiano utakaofanyika jijini Lusaka, unatarajiwa kuwa wa aina yake haswa kutokana na kocha wa Yanga George Lwandamina kuwa raia wa Zambia. Mbali na uraia lakini pia kocha huyo kabla ya kutua Yanga alikuwa akiinoa klabu ya Zesco United inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia hivyo kumfanya kuwafahamu zaidi Zanaco.

No comments:

Post a Comment