Friday, March 10, 2017

SAMATTA AWA GUMZO ULAYA.

KLABU ya Genk bado wana hofu na Gent kuelekea katika mchezo wao wa mkondo wa pili hatua ya 16 bora ya Europa League pamoja na ushindi mnono wa mabao 5-2 waliopata jana. Katika mchezo huo, mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta alifunga mabao mawili katika dakika ya 41 na 72 na kuipa Genk ushindi huo mnono wa mkondo wa kwanza. Hata hivyo, meneja wa Genk Albert Stuivenberg amesema pamoja na ushindi huo lakini hawapaswi kubweteka kwani wapinzani wao Gent bado wanaweza kubadili matokeo hayo na kutolewa mfano Barcelona. Barcelona walitinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya juzi kufuatia kuifunga Paris Saint-Germain kwa mabao 6-1 katika mchezo wa marudiano uliofanyika Camp Nou baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa mabao 4-0 kule Ufaransa. Stuivenberg amesema waliona kitu cha kipekee kwa Barcelona, lakini kinaweza kutokea tena katika soka hivyo lazima wajindae kikamilifu kuhakikisha wanalinda ushindi wao kwenye mchezo wa marudiano.

No comments:

Post a Comment