Friday, March 10, 2017

KANE NDIO MCHEZAJI BORA WA FEBRUARI.

MSHAMBULIAJI wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu baada ya kufunga mabao manne katika mechi tatu alizocheza. Kane ndio anaongoza kwa ufungaji katika ligi akiwa na mabao 19, akimzidi bao moja Romelu Lukaku wa Everton na mabao yake yameisaidia Spurs kukaa kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi nyuma ya vinara Chelsea. Akizungumza na wanahabari, Kane amesema ni heshima kubwa kutwaa tuzo hiyo na umekuwa mwezi mzuri kwake pamoja na timu yake. Kwa upande mwingine meneja wa Manchester City, Pep Guardiola ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi kufuatia kuisaidia timu yake kushinda mechi tatu mwezi uliopita, ikiwemo ile ya mabao 4-0 dhidi ya West ham United, mabao 2-1 dhidi ya Swansea City na mabao 2-0 dhidi ya Bournemouth. Naye mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard ametwaa tuzo ya bao bora la mwezi ambalo alifunga katika mchezo walioshinda mabao 3-0 dhidi ya Arsenal.

No comments:

Post a Comment